Monday, February 5, 2018

MTOTO MCHANGA ALIYEIBIWA MBEYA APATIKANA , KAMANDA MPINGA ATOA ONYO

Tokeo la picha la PICHA YA KAMANDA MPINGA MBEYA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA ametoa wito kwa jamii kuondokana na tamaa ya kutaka utajiri kwa njia zisizo halali kwa kujihusisha na uhalifu na badala yake watafute shughuli halali kwa ajili ya kujipatia kipato.

Kamanda mpinga ametoa onyo hilo alipokua akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo ameeleza kuwa Mnamo tarehe 03 Februari, 2018 majira ya saa 12:00 Mchana huko maeneo ya mtaa wa Mponja – Uyole, Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Viongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya walifanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la HAPPY CHARLES [24] Mama Lishe, Mkazi wa Airport ya Zamani akiwa na mtoto mchanga jinsia ya kike aliyemuiba katika  Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Awali mnamo tarehe 01 Februari, 2018 majira ya saa 04:00 usiku huko katika wodi ya watoto Hospitali ya Mkoa wa Mbeya iliyopo Kata ya Forest Mpya, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la SARAH MWASANGA [35] Mkazi wa Iganzo akiwa katika wodi ya wazazi Hospitalini hapo baada ya kujifungua mtoto wa kike aligundua kuibiwa kwa mtoto huyo na mtu asiyefahamika.

Kutokana na tukio hilo, uongozi wa Hospitali hiyo ulitoa taarifa kituo kikuu cha Polisi [Central] na ndipo upelelezi kuhusiana na tukio hilo ulianza kufanyika.


Taarifa za siri zilipatikana na kubainisha kuwa huko maeneo ya Airport ya zamani kuna mama mmoja aitwaye HAPPY CHARLES [24] Mkazi wa Airport ambaye hapo awali alikuwa akimdanganya mume wake aitwaye CHILUBA PETER, Dereva Taxi Hospitali ya Rufaa Mbeya na Mkazi wa Airport kuwa ni mjamzito na kwamba amejifungua mtoto wa kike tarehe 31 Februari, 2018 na ndipo ufuatiliaji wa kuwapata watu hao ulianza.

No comments: