Sunday, May 25, 2014

CCM YACHANA MBUGA MKOANI SINGIDA, YAELEZEA MIPANGO YAKE YA MAENDELEO KWA WANANCHI

19 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mjini Singida wakati alipowahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja vya Peoples mjini humo ambapo mawaziri mbalimbali wamehudhuria na kuwaelezea wananchi mpiango ya serikali katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 katika mipango ya maendeleo, Mkutano huu ulikuwa ni wa mwisho kabla ya kumalizia ziara yake katika mkoa  wa Singida hapo kesho kabla ya kuendelea na ziara hiyo katika mkoa wa Manyara keshokutwa , Ambapo katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye, Mawaziri waliohudhuria katika mkutano huo mkubwa ambao umerushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star Tv ni Dr. Charles Tizeba naibu waziri wa uchukuzi, Amos makala Naibu Waziri wa Maji, Mwigulu Nchemba naibu waziri wa Fedha na Uchumi na, Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Stephen Wasira Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na Adam Malima Naibu waziri wa Fedha na Uchumi  na viongozi mbalimbali wa kitaifa na mkoa wa Singida.30 29 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Singida 27 
Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Singida Mashariki Bw. Andrew Andalu akipongezwa na Mh. Stephen Wasira  mara baada ya  alipotangaza kukihama chama cha CHADEMA na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara mjini Singida, kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida mjini Khamis Nguli na Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu wa CCM.

CHADEMA IRINGA MJINI WATIMULIWA KATIKA MAZISHI YA DEREVA BODA BODA , WASEMA WAO SI CHAMA CHA SIASA

” Huyu mwenzetu mbali ya kupata ajali ya  pikipiki kwa siku zaidi ya nne  sasa alikuwa amelezwa  Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na madereva tulianza kuchangishana  ili kumfanyia rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili …..sasa kama Chadema ambao  leo wanakuja na bendera wapo kwanini  wasingetoa usafiri wa kwenda Muhimbili kama si kutaka kuonekana sasa baada ya kifo”

MBEYA CITY FC WAICHACHABANGA ACADEMIE 3-2, MWAMBUSI AWASIFU WANANDINGA WAKE: CECAFA NILE BASIN CUP


IMG_7961 IMG_8009 IMG_8039 IMG_8061
WAGONGA Nyundo wa jijini Mbeya,  Mbeya City fc jana walitoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi katika mchezo wa kundi B wa michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea mjini Khartoum nchini Sudan.
 
Mbeya City fc waliofika Khartoum siku moja kabla ya mechi walianza kufungwa bao katika dakika ya 10 baada ya Rashid kumtungua kipa wao, lakini walirudi mchezoni baada ya Paul Nonga kusawazisha bao hilo dakika 5 baadaye. 
 
Dakika ya 27, nahodha wa Mbeya City fc, Mwegane Yeya kama ilivyo kawaida yake alifunga bao la pili kwa njia ya kichwa. Them Felix `Mnyama` alihitimisha karamu ya mabao dakika ya 37 baada ya kufunga bao safi na kuwapeleka Mbeya City mapumziko wakiwa na furaha.

Rais Kikwete amjulia hali mama mzazi wa Zitto Kabwe

D92A5200 D92A5199
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mama Mzazi wa Mbunge  wa Kigoma Kaskazini  kwa tiketi ya CHADEMA Zitto Zuberi Kabwe aliyelazwa katika wodi ya wagonjwa wenye kuhitaji uangilizi maalumu (ICU) hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

Mahakama yamkosoa rais Banda Malawi

HE_Joyce_Banda_President_of_Malawi_7163532051_f1029.jpg
Mahakama kuu nchini Malawi imetoa hukumu dhidi ya jaribio la rais Joyce Banda kupiga marufuku matokeo ya shughuli ya uchaguzi wa urais na ubunge.

Mahakama imeiagiza tume ya uchaguzi nchini humo kuendelea na shughuli ya kuhesabu kura.
Mahakama italiangazia upya tangazo la rais Banda kwamba uchaguzi huo haufai kwa kuwa ulikumbwa na udanganyifu mkubwa.

Bi. Banda yuko katika nafasi ya pili kulinga na matokeo yaliotangazwa na kwamba ndugu ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Peter Mutharika ndio anayeongoza.(P.T)
Chanzo:bbc

SHANGWE TUPU; REAL MADRID BINGWA ULAYA, YAITANDIKA ATLETICO MADRID 4-1


Nahodha wa Real Madrid, Iker Casillas akiwa ameinua Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwafunga jirani zao, Atletico mabao 4-1 usiku huu Uwanja wa Luz mjini Lisbon, Ureno. Hilo linakuwa taji la 10 la michuano hiyo kwa Real.
Uplifting: Ronaldo gets his hands on the trophy in Lisbon after Real's extra time victory
Mfungaji wa bao la nne la Real, Cristiano Ronaldo akiwa ameinua Kombe
Landmark: Real Madrid's players celebrate their 10th European Cup triumph
Kikosi cha Real Madrid kikifurahia na Kombe hilo

Watanzania kuleni nyama ya panya.

panyaclip 0786e

Watanzania wameshauriwa kufuga na kula panya aina ya ndezi wakieleza kuwa nyama hiyo haina mafuta mengi, ikiwa pia na virutubisho muhimu na vilivyo adimu.

Rai hiyo imetolewa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wataalamu hao walisema kuwa ili kukabiliana na uharibifu wa kuchoma moto misitu kwa ajili ya kuwatafuta wanyama hao, ni vyema wananchi wakaanza kuwafuga kwa kuwa nyama yao ina ladha nzuri na ni laini.

Mhadhiri Mwandamizi wa SUA, Idara ya Uzalishaji, Mirende Matiko alisema kuwa ingawa wanyama hao wanafugwa kwa wingi katika nchi za Afrika Magharibi, hapa nchini ufugaji wake unakabiliwa na changamoto nyingi.
"Wakulima wetu hapa tunawapa wafuge, siku chache baadaye ukienda utaambiwa walikufa, lakini ukiwauliza majirani wanakuwambia 'jamaa aliwachinja', ni sawa na kumpa mkulima mbegu halafu anakula," alisema Matiko.

Akizungumzia namna nyama hiyo inavyoliwa, Matiko alisema: " Nyama yake ina viinilishe vingi, yanatupwa manyoya na miguu yake tu, vitu vingine vyote vinaliwa. Tena utumbo ndiyo mtamu sana, si unajua wanakula nyasi tu."

Alisema wanyama hao wana faida nyingi kiuchumi ikiwamo kuongeza pato la kaya, kuchangia uwindaji endelevu, kutunza bioanuwai pia nyama yao ni gharama nafuu, ikilinganishwa na nyingine.
"Mtu akitaka kufuga wanyama hao anatakiwa kuwa na banda madhubuti lenye ubora, chakula na maji safi yawepo bandani muda wote na upandishaji ufanyike katika muda mwafaka," alisema.
Mhadhiri huyo alitoa hadhari kwa wafugaji akiwataka kuwakamata wanyama hao kwa umakini kutumia chandarua, kuepuka kusababisha majeraha.

Ndezi ni jamii ya nungunungu na pimbi, wakiwa wa aina mbili, ambapo wadogo huwa na uzito wa kati ya kilo nne hadi sita na wakubwa hufikia hadi kilo tisa. Wanyama hao hupendelea kuishi kwenye maeneo yanayolimwa mashamba ya miwa, ulezi na mpunga.
Hata hivyo, Dk Loth Mulungu alisema kuwa wawindaji wa ndezi porini husababisha madhara makubwa ikiwamo uchomaji wa misitu, uharibifu wa bioanuwai, kukanyaga mazao mashambani na upotevu wa muda.

Mmoja wa watazamaji waliotembelea Banda la SUA, Elizabeth Maro alisema kuwa ingawa kwa muda mrefu amesikia watu wakila mnyama huyo. Binafsi hawezi kula nyama yake kwa kuwa anaamini hana tofauti na panya wengine.

"Siwezi kumla kwa namna yoyote, huyu ni panya tu ndiyo maana hata jina lake kwa Kiingereza anaitwa 'canerat', maana yake panya mla miwa," alisema.Ipyana Mwambungu alisema mnyama huyo ameadimika katika baadhi ya mikoa kutokana na watu wengi kuipenda nyama yake.
"Kuna baadhi ya maeneo kule Kilimanjaro huwezi kuwaona tena ndezi, wakati zamani walikuwa wengi sana," alisema.
CHANZO MWANANCHI

Kova: Tumewanasa viongozi wa ‘Mbwa Mwitu’

kova 89b8e

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watu sita wanaodaiwa ni viongozi wa kundi la 'Mbwa Mwitu' linalojihusisha na vitendo vya uvamizi na uporaji wa mali za watu kwenye nyumba na maduka jijini humo.

Kamanda wa Polisi kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kutokana na kukamatwa kwa viongozi hao na kupatikana kwa taarifa za makundi hayo jeshi lake litafanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa hadi wahusika wote wakamatwe.

"Hawa viongozi tunao, tumeshawahoji na wamekiri ni kweli wamekuwa wakijihusisha na vitendo hivyo kwa kutumia makundi yao," alisema Kova na kuongeza: "Sisi tunaanza kuwasaka hao vijana kwa sababu tumeshapata taarifa za kutosha kutoka kwa wenzao...tunafahamu wapi pa kuwapata."

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Athuman Said (20), Joseph Ponela na Clement Peter (25) wakazi wa Kigogo, Roma Vitus (37), Mwanshishe Adam(37) na Daniel Peter (25)wakazi wa Temeke.
Taarifa hiyo imekuja siku moja baada ya kusambaa kwa taarifa za kundi hilo la vijana zaidi ya 300 kuvamia mitaa mbalimbali ya jiji hilo, kupora mali na kujeruhi watu.
Kamishna Kova alisema kuwa jeshi lake lilifanikiwa kuwakamata viongozi hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema akisisitiza kwamba hatua inayofuata ni kuwasaka vijana wanaowatuma kufanya uhalifu huo.

"Hii itakuwa operesheni endelevu tunayoianza mwezi huu hadi mwezi Julai mpaka tuhakikishe tumewakamata wahalifu hawa na tatizo hili limetokomea,"alisema Kova kwa msisitizo.

Alisema jeshi lake limejipanga kukabiliana na wahalifu hao na kuwa wananchi waache kuwa na hofu kutokana na taarifa za uvumi zinazosambazwa kwenye mitandao kuhusu uhalifu unaofanywa na vijama hao.
"Ningependa kuwatoa hofu wananchi kuhusiana na uvumi unaoendelea kwenye mitandao...tunaomba wananchi wawe watulivu waendelee na shughuli zao kama kawaida. Jeshi langu limejipanga vizuri kuwadhibiti hao vijana. Hao vijana hawana uwezo wa kutushinda sisi" alisema Kova

Kamanda huyo aliweka wazi kuwa askari wa kutosha wa doria wameshapangwa maeneo ambayo yametajwa kuwa na mlipuko wa makundi hayo.Maeneo hayo ni pamoja na Kigogo, Manzese, Magomeni na Mbagala.
CHANZO MWANANCHI